KOMBE LA KAGAME |
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo hii imekubali kuwa wenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa
Afrika Mashariki na Kati ngazi ya klabu maarufu kama Cecafa Kagame Cup.
Cecafa ambao ndio wamiliki
wa mashindano haya watatoa mialiko kwa klabu zenye sifa ya kushiriki na
wakipokea uthibitisho wa ushiriki wao watatoa orodha ya klabu shiriki na ratiba
ya michuano hiyo.
Michuano hii
inatarajiwa kuafanyika nchini kuanzia Julai 11 hadi Agosti 2, 2015.
0 COMMENTS:
Post a Comment