![]() |
| WAKIWA WAMEMUWEKA CHINI YA ULINZI, MWANGALIE AMEKAA CHINI. SHABIKI MWENYE SHATI LA KIJANI (KUSHOTO) AKIWAPOZA WAACHE HASIRA.... |
Wachezaji wa kikosi cha Taifa Stars, leo wametoa
kali ya mwaka baada ya kushuka kwenye basi lao na kumkamata shabiki na kumpa kibano.
Wachezaji hao walilazimika kushuka na kumkimbiza
shabiki mmoja aliyeelezwa kuwa ni dereva bodaboda.
Tukio limetokea leo katika makutano ya barabara
ya Uhuru na ile inayotokea Kariakoo kwenda Gerezani.
![]() |
| WAKIMKIMBIZA... |
Wachezaji hao waliteremka kwenye gari hilo na kumkimbiza wakiongozwa na kipa
Deo Munish.
Pamoja na “kumpasha” kidogo, walimuweka chini ya
ulinzi na baadaye wakamuachia.
Kabla ya tukio hilo, siku moja kabla mashabiki
walilishambulia basi la Taifa Stars na kuvunja kioo.
![]() |
| WAKIRUDI KWENYE BASI LAO... |
Hali hiyo inatokana na mashabiki kuchukizwa na
Stars kupoteza mechi dhidi ya Misri kwa mabao 3-0 lakini pia kikosi hicho
kufanya vibaya katika michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini.










0 COMMENTS:
Post a Comment