Mshambuliaji
mpya wa Yanga, Malimi Busungu, ameanza kuonyesha makali yake uwanjani baada ya
kumpa wakati mgumu beki na nahodha wa Simba, Hassan Isihaka wakati wa mazoezi
ya timu ya taifa, Taifa Stars, jana.
Katika mazoezi
hayo, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Gymkhana, Posta jijini Dar es Salaam,
Kocha Mkuu wa Stars, Mart Nooij alianza kwa programu ya kukimbia mbio fupi na
baadaye ndefu iliyotumia dakika 10.
Baadaye
vilipangwa vikosi viwili na ndipo Busungu na Isihaka wakapangwa tofauti,
Busungu alikuwa namba tisa na alikuwa akikabwa zaidi na Isihaka pamoja na Joram
Mgeveke.
Busungu
aliyetua Yanga hivi karibuni akitokea Mgambo, alikuwa msumbufu kwa beki huyo
ambapo alifanikiwa kumtoka mara kadhaa na kupiga mashuti mbele yake.
Licha ya
mshambuliaji huyo kufanya vitu vyote hivyo, hadi filimbi ya mwisho inapulizwa
na Nooij, hakupata bao katika mazoezi hayo.
Aidha, katika
mazoezi hayo, Nooij aliwabadilisha nafasi za uwanjani Deus Kaseke wa Yanga na
Rashidi Mandawa wa Mwadui.
Kaseke ambaye
wakati akiwa Mbeya City alikuwa akitumika kama kiungo wa pembeni, jana
alipangwa namba nane huku Mandawa akicheza namba 11 wakati alipokuwa Kagera
Sugar alikuwa akitumika katika nafasi ya mshambuliaji wa kati (namba tisa).
Alipoulizwa
Kaseke kuhusiana na kubadilishwa namba alisema: “Mimi ni kama mfungwa ambaye
hachagui gereza, hivyo kubadilishwa namba kwangu ni moja ya changamoto
nitakazoweza kukutana nazo Yanga.
“Nina uwezo wa
kucheza nafasi zote za ndani ya uwanja isipokuwa kipa pekee, ni vema mashabiki
wa soka wakalifahamu hilo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment