KESSY (WA PILI KULIA) AKWIA NA WENZAKE KATIKA MAZOEZI YA STARS, JANA. |
Timu ya taifa
ya Tanzania, Taifa Stars, imeondoka jana kuelekea jijini Addis Ababa nchini
Ethiopia kuweka kambi lakini Kocha Mkuu Mart Nooij amefanya mabadiliko kadhaa
katika kikosi chake.
Nooij
amemuondoa kikosini winga Haruna Chanongo wa Stand United na kuwajumuisha Amri
Kiemba aliyekuwa Simba na Hassan Kessy wa Simba ambao hawakuwepo kabisa
kikosini.
Stars itaweka
kambi Addis Ababa kwa muda wa wiki moja kisha kuelekea nchini Misri kukipiga na
timu ya taifa hilo Juni 14, 2015 katika kuwania kufuzu michuano ya Mataifa
Afrika 2017.
Akizungumza
kabla ya kuondoka nchini, jana, Nooij alisema wachezaji waliosafiri kuelekea
Ethiopia ni; Deogratias Munishi, Aishi
Manula, Mwadini Ali, walinzi Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Erasto Nyoni, Nadir
Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji, Salum Mbonde na Juma Abdul.
Wengine ni
Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, Salum Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said
Ndemla, washambuliaji Saimon Msuva, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana
Samatta, Mrisho Ngassa na Juma Luizio.
0 COMMENTS:
Post a Comment