Sakata la kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ limechukua
sura mpya baada ya Simba kutaka vyombo vya dola kuingilia.
Simba imetaka vyombo vya dola kuingilia na kufanya
uchunguzi ili kuangalia nani aliyefanya fojali kati ya klabu hiyo na kiungo
huyo.
“Sasa tunaomba vyombo vya dola viingilie, wafanye
uchunguzi na mwisho kuwe na ukweli. Sisi tunajiamini na tunataka kusafishwa
katika hili.
“Ndiyo maana tunasisitiza uchunguzi ufanyike kupitia
wataalamu wa vyombo vya dola ili kupata uhakika,” alisema Msemaji wa Simba,
Haji Manara.
Messi amekuwa akilalama kwamba mkataba wake una miaka
miwili na unaisha baada ya kwisha kwa msimu wa 2014-15.
Simba wanapinga na kusema waliingia naye mkata wa miaka mitatu na unamalizika 2015-16. Jambo ambalo limezua malumbano ya kila aina.
Hata hivyo, Simba wamekuwa wakidai wao wana mkataba
halisi ambao waliingia na Messi, wakati kiungo huyo amekuwa hana mkataba
orijono, anamiliki kopi pekee ambayo inaonyesha ni mkataba wa miaka miwili.
0 COMMENTS:
Post a Comment