Mbio za Bagamoyo
Historical Marathon zilizofanyika jana Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani
zilitiafora kufuatia mchuano mkali ulioshirikisha taasisi na raia wa mataifa
mbalimbali.
Katika michuano hiyo
Klabu ya Mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF) ambao huundwa na wafanyakazi wa mfuko
huo kuwagalagaza wengine na wengi kuwemo kwenye kumi bora katika mbio za
kilometa 5,10, na 21.
Wengine waliofanya
vizuri kwenye mbio hizo ni raia wa kigeni kutoka barani Ulaya, Asia, Amerika na
kwingineko.
Katika mbio hizo
mshindi wa kwanza alikuwa Gabriel Gerald akifuatiwa na Panuel Mkungwa ambapo
mshindi wa tatu alikuwa Dikson Marwa.
Washiriki wa mbio hizo
walinufaika na kupimwa bure afya zao na madaktari kutoka NHIF nakupatiwa majibu
yao hapohapo na kupatiwa ushauri wa kuboresha afya zao.
Akifunga mashindano
hayo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk. Shukuru Kawambwa
aliwapongeza washiriki wote kwani wameboresha afya zao na kuutangaza Utalii wa
mji huo wa kale (Bagamoyo) jambo ambalo lilikuwa dhumuni la mbio hizo.







0 COMMENTS:
Post a Comment