Na Fahad Ally, Mwanza
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema anashangazwa suala
la kocha mpya wa Simba kuwa gumzo sana na kusisitiza, watu wavute subira.
Akizungumza
na SALEHJEMBE jijini hapa, Hans Poppe amesema Simba iko katika hatua ya mwisho
kumalizana na kocha huyo.
“Vuteni
subira kidogo, mambo yanakwenda kwa mpangilio. Si lazima kuwe na haraka kiasi
hicho, tutawataarifu bila ya shida,” alisema.
“Najua
mna hamu ya kumjua lakini ni suala ambalo linahitaji umakini. Najua nilishawaeleza
tokea mwanzo kwamba anatokea Uingereza,” alisema.
Tokea kuondoka
kwa Goran Kopunovic kumekuwa hakuna uhakika Simba inamchukua nani huku suala
hilo likiendelea kuwa siri kubwa.







0 COMMENTS:
Post a Comment