Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, ameanza
kukisuka kikosi chake kwa kuanza kuisuka kombinisheni mbili ya ushambuliaji
katika kuhakikisha safu hiyo inakuwa tishio msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi
ya Mabingwa Afrika.
Maandalizi hayo yanawahusisha wachezaji wapya
waliosajiliwa na timu hiyo ambao ni Deus Kaseke, Malimi Busungu na Benedicto
Tinoco.
Kocha huyo alionekana akitengeneza kombinesheni
hizo wakati timu hiyo ilipocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers
kwenye Uwanja wa Karume juzi jijini Dar.
Kocha huyo alimuanzisha Busungu aliyecheza namba
10 na Mliberia, Kpah Sherman aliyecheza namba 9 ambao walionekana kucheza kwa
kuelewana.
Kombinesheni hiyo, ilionekana kuelewana pale
Busungu alipomtengenezea nafasi ya kufunga Sherman baada ya kugongeana ndani ya
18 kabla ya Mliberia huyo kufunga.
Kombinesheni ilionekana kunoga pale Busungu
alipofunga bao la pili kwa kumchambua kipa akitumia krosi ya Sherman kabla ya
kuzitingisha nyavu za Rangers.
Kipindi cha pili, kocha aliijaribu kombinesheni
nyingine ya ushambuliaji kwa kumtoa Sherman na kuingia Mrundi, Amissi Tambwe
aliyecheza pamoja na Busungu.
Washambuliaji hao, walionekana kuelewana kwa
kutengenezeana nafasi za kufunga licha ya kushindwa kuzitumia vema nafasi hizo.
“Najaribu kombinesheni tofauti za wachezaji na
pia nawapa mbinu huku nikiendelea kuwapa mazoezi ya nguvu na stamina,” alisema
Pluijm mara baada ya mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment