Kocha Mkuu wa Yanga,
Hans van der Pluijm leo aliamua kumpa mambo kadhaa ya ufundi kipya mpya wa
Yanga, Benedict Tinocco.
Pluijm ambaye aliwahi
kuwa kipa wa timu ya taifa ya Uholanzi na Pondamali aliyewahi kuidakia Taifa
Stars, walitumia zaidi ya dakika tano wakirekebisha makosa kadhaa ya Tinocco.
Pluijm aliamua kusogea
karibu na kusaidiana na Pondamali kuhusiana na makosa hayo ya Tinocco ambaye
ndiye amejiunga na Yanga akitokea Kagera Sugar.
Yanga imefanya mazoezi
yake leo kwa siku ya pili mfululizo baada ya kuanza upya mazoezi, jana.
0 COMMENTS:
Post a Comment