June 11, 2015


Simba Sports Club
Taarifa kwa vyombo vya habari
Kikao cha kamati ya utendaji ya club ya simba kilichokutana jana tarehe 10/06/2015, pamoja na mambo mengine kilijadili suala la mchezaji wa Simba Ramadhan Yahya Singano na kuamua yafuatayo:

Kwa kuwa Mchezaji Ramadhan Yahya Singano alivunja makubaliano yaliyoamuliwa katika kikao cha pamoja kati ya club ya Simba, mchezaji mwenyewe, Sputanza na secretarieti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kutozungumzia yaliyojadiliwa na kupendekezwa kwenye kikao kwa kuyazungumza kwenye vyombo vya habari kwa kusema yeye ni mchezaji huru.

Klabu ya simba imeamua kutokufanya mazungumzo na mchezaji huyo kwa sasa kwa kuwa bado ina mkataba naye ambao utaisha 01/07/2016. 

Hata hivyo Klabu itakuwa tayari kufanya naye mazungumzo pindi muda mwafaka utakapofika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mikataba.

Ni matarajio yetu mchezaji Singano ataheshimu maamuzi hayo na mkataba ambao pia upo TFF na kwenye mtandao TMS.


Imetolewa na 
Evans Aveva
Rais 
Simba Sports Club

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic