Na Saleh Ally
HALI
ilivyo katika kikosi chetu cha Taifa Stars lazima tukubali kwamba si nzuri na
hakuna matumaini ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika au lile la timu za nyumbani
maarufu kama Chan.
Matumaini
hakuna kutokana na hali halisi, kwamba hatuna mwendo mzuri, si timu inayosomeka
kwa Watanzania kwamba inataka kufanya jambo.
Wakati
yote hayo yakiwa yamejazana katika vichwa vya Watanzania, Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) limefanya hafla iliyokuwa na mambo mengi, si vibaya kuyapongeza.
Hafla
hiyo iliyofanyika juzi, TFF iliwatuza watu mbalimbali waliopambana katika
kusaidia soka ya Tanzania tokea nchi yetu ilipojiunga na FIfa miaka 50
iliyopita.
Hongera
TFF kwa kuwakumbuka wachezaji na viongozi wa zamani. Hongera sana kwa TFF kwa
kuwajali wadhamini wao kwa miaka nenda rudi, najua hamkuwaweka Serengeti au SBL
kwa kuwa mko na Kilimanjaro na TBL, lakini nao walistahili pongezi kwa kuwa si
lahisi kuwang’oa katiaka historia.
SBL
au Serengeti ndiyo walikuwa changamoto hadi TBL wakiwa na Kilimanjaro wakaona
Taifa Stars inaweza kudhamini. Bado nao walistahili kupongezwa pia.
Pia
hongera TFF, mmewakumbuka waandishi wakongwe wa enzi zile. Sitaki kuwalaumu
mliwasau wa sasa ambazo wanawasaidia kusukuma gurudumu lenu ambao pia walipaswa
kuunganishwa, hiyo si ishu kubwa.
Lakini
bado niliona mlipaswa kuwapongeza wadhamini wa sasa kama vile Bin Slum Tyres
ambao wamefanya mambo makubwa kwa kudhamini timu tatu katika ligi moja, tena
timu ambazo hazikuwa na majina makubwa na mbili kati ya hizo, ndiyo zilikuwa
zimepanda daraja.
Huenda
Bin Slum Tyres, ndiyo walikuwa wadhamini jasiri kuliko wengine wote baada ya
kujitolea kuwekeza kwa timu zilisizoaminika. Utaona udhamini huo ulivyokuwa
changamoto na kila timu ikapambana isiteremke daraja, kweli zote tatu yaani
Mbeya City, Stand United na Ndanda FC zimebaki Ligi Kuu Bara.
Lakini
nilichokuwa nakilenga zaidi ni ile ishu ya uzinduzi wa jezi mpya ambao ulikuwa
ni sehemu ya shughuli hiyo. Zimezinduliwa jezi, ambazo kwangu sioni kwama kuna
haja ya kuzikagua sana, tunaweza kwenda nazo.
Kila
mmoja wetu aliye makini anaweza kujiuliza kuhusiana na jezi hizo mpya, kwamba
je, ndiyo suluhisho la matatizo yetu kwa kuwa tunajua tuna kikosi dhaifu?
Stars
haionyeshi kama ina nia ya dhati ya kufuzu au kufika mbali. Haionekani kama ina
kikosi chenye nguvu ya kusonga, zaidi wote tunawabebesha mzigo baadhi ya
wachezaji wachache kama Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwamba ndiyo
watakuwa msaada. Tutawaonea.
Lazima
tukubaliane, jezi inaweza ikawa ni sehemu ya mabadiliko madogo sana na huenda
yasiwe na tija hata kidogo kama Stars itaendelea kuboronga au kuwa timu ya
kubahatisha.
Lazima
tukubaliane, Watanzania wanataka kuona timu yao inacheza Afcon au Chan, halafu
ifuatie Kombe la Dunia. Suala la jezi ni chembe ndogo ambayo kama ingekuwa ni
kidonda, basi ni kile kisichoweza kumzuia mchezaji au mkimbiaji kushiriki
mashindano.
Tumeona
jezi zimezinduliwa, lakini hiyo bado haijabadilika hata kidogo nguvu na fikra
ya nini cha kufanya ili tucheze michuano hiyo mikubwa.
Hongera
TFF kwa kubadili jezi, ni wazo zuri lakini bado hiyo si ndoto ya Watanzania.
Wanachotaka ni kikosi cha TAifa Stars kufanya vizuri na kufikia ndoto sahihi
ambayo ni kushiriki michuano mikubwa ya Afrika.
Tanzania
inaweza kushiriki Afcon na Chan kwa kuwa imewahi kushiriki michuano yote hiyo.
Hivyo naweza kusema kwa uhakika, ndoto wanazoota Watanzania si za Alinacha, ni
kitu kinachowezekana. Hii ina maanisha, ni deni kwa uongozi wa Jamal Malinzi
kwamba hata ajitahidi vipi, kama Stars haitafanya vema, basi kila kizuri
ikiwemo kubadili kwa jezi, hakutakuwa na tija hata chembe.
0 COMMENTS:
Post a Comment