June 5, 2015


Uongozi wa Klabu ya Ndanda umetangaza aina ya wachezaji wanaowahitaji kutokana na mapendekezo ya kamati yao ya usajili.


Uongozi huo umesema kuwa umeamua kuongeza wachezaji 11 ili kuziba mapengo na aina ya nafasi ambazo zilionekana kuwa na upungufu msimu uliopita ambapo ni makipa wawili, straika wawili, mabeki wa kati wawili, kiungo mmoja, winga mmoja pamoja na mabeki watatu.

Ofisa habari wa timu hiyo, Idrisa Bandari amesema hili kuwa bado hawana uhakika wa kuwapata wachezaji hao na ndiyo maana hawawezi kutaja majina kwa sasa.


“Tungekuwa na uhakika wa kuwapata wachezaji  tunaowahitaji, tungewataja majina, lakini kwa kuwa bado hatujafanya nao mazungumzo tutawaweka wazi baadaye,” alisema Bandari.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic