Msafara
wa timu ya Taifa ya Tanzania (taifa Stars) inayodhaminiwa na kampuni ya bia ya
Kilimanjaro Premium Lager tayari umewasili salama katika eneo la Borg El Arab
jijini Alexandria na kufikia katika hoteli ya Panacea tayari kwa mchezo wake wa
kesho.
Taifa
Stars ambayo ilikuwa kambini nchini Ethiopia kwa takribani wiki moja, iliondoka
jana usiku Addis Ababa na kuwasili uwanja wa ndege wa Cairo majira ya saa
8 usiku, kisha kuunganisha kwa usafiri wa basi mpaka Borg El Arab takribani
masaa matatu.
Kocha
mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij, atakiongoza kikosi chake katika mazoezi ya
mwisho leo saa 1 usiku katika uwanja wa Borg El Arab kwa saa za Misri, sawa na
saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Akiongelea
mchezo wa kesho, Nooij amesema anashukuru kikosi kimefika salama nchini Misri
na kipo katika hali nzuri, vijana wana ari na morali ya hali ya juu, anaamini
kesho timu itfanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya wenyeji Misri.
Nooij
amesema mchezo wa kesho ni muhimu kwake, na kikosi chake kitacheza mpira wa
kasi na pasi za haraka haraka, huku safu ya ushambuliaji ikihakikisha inatumia
vizuri nafasi itakazozipata.
Aidha
kuelekea katika mchezo huo wa kesho, kiungo Amri Kiemba ameungana na wachezaji
wengine waliokuwa kambini Addis Ababa kuchukua nafasi ya Mrisho Ngasa ambaye
alishindwa kuungana na timu kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wake.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia tayari amewasili
jijini Alexandria kwa ajili ya kuipa sapoti Taifa Stars katika mchezo huo wa
kesho.
Mchezo
kati ya Misri na Tanzania utachezwa kesho saa 2 usiku kwa saa za Afrika
Mashariki na kati katika uwanja wa jeshi la Misri (Borg El Arab) uliopo
takribani kilometa 70 kutoka jijini Alexandria na kilometa 200 kutoka jiji la
Cairo.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)








0 COMMENTS:
Post a Comment