Na Fahad Ally, Mwanza
Timu
ya watoto wa Kinondoni imefanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuichapa
Mara kwa mabao 2-1 ya mikwaju ya penalti.
Katika
mechi hiyo safi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, leo, timu hizo zilimaliza
dakika za kawaida bila ya bao na kulazimika kuingia katika changamoto wa
mikwaju ya penalti.
Mara
walipata mkwaju mmoja kupitia nahodha wake na Kinondoni wakafunga miwili huku
makipa wa pande zote mbili wakiokoa mikwaju miwili.
Kinondoni
ilionekana kuwa na nafasi nzuri kuanzia kipindi cha kwanza pia cha pili, lakini
hawakuzitumia vizuri.
Alliance
na Ilala pia ya Dar es Salaam, ndiyo zimeingia fainali katika michuano hii ya
kusaka timu ya watoto chini ya miaka 13 ambao wataingia kambini kwa ajili ya
kuwaandaa vijana waliobainika kuwa na vipaji.
Programu
hiyo imeandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Rais wake, Jamal
Malinzi alikuwa uwanjani hapo kushuhudia mechi hizo mbili za kuvutia na ndiye alikuwa mgeni rasmi.
Fainali,
ndiyo inaendelea.







0 COMMENTS:
Post a Comment