June 11, 2015

Mshambuliaji Laudit Mavugo ambaye anatarajia kujiunga hivi karibuni na kikosi cha timu hiyo, amesema zaidi ni mtu wa familia.


Mavugo amesema maisha yake pamoja na soka kuwa namba moja katika moyo wake, baada ya hapo ni familia yake.

“Napenda sana familia yangu, ndiyo maana umeona hizo picha. Nitakuwa na mama (mpenzi) au mtoto.

“Wakati mwingine ninakuwa na rafiki zangu, lakini si mtu anayependa mambo mengi,” alisema alipohojiwa na moja ya magazeti ya Burundi, hivi karibuni.


Taarifa zinaeleza kwamba Mavugo ambaye sasa anakipiga Vital’O tayari ameishasaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic