Rais
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema lengo la kuandaa
michuano ya watoto chini ya 13 inayomalizika leo jijini hapa, ni kushiriki
fainali za Michezo ya Olimpiki itakayofanyika jijini Tokyo, Japan.
Akizungumza
kabla ya mchezo wa fainali ya michuano hiyo, Malinzi alisema vijana wanaocheza
michuano hiyo watakuwa na nafasi ya kucheza timu bora ya taifa ya vijana chini
ya miaka 17.
Amesema
watapata nafasi ya kushiriki michuano ya mbalimbali ya watoto.
“Mwakani
tutaandaa michuano ya watoto chini ya miaka 14. Watatunzwa watakaoteuliwa wenye
vipaji na baada ya hapo watakuzwa vizuri ili kuingia kwenye timu hiyo chini ya
miaka 17.
“Tunaamini
timu ikishiriki Olimpiki, itatuzaidia kushiriki michuano mingine mikubwa kama
tutaendelea nao,” alisema.
Katika
mechi ya mshindi wa tatu, Kinondoni imeishinda Mara kwa mabao 2-1. Michuano
hiyo haina kombe kwa kuwa lengo ni kusaidia kupata timu.







0 COMMENTS:
Post a Comment