| ABOAGYE AKIPAMBANA NA OKWI KATIKA MAZOEZI YA SIMBA |
Mshambuliaji Aboagye Geirson raia wa Ghana aliyekuja kufanya
majaribio ya kucheza soka la kulipwa Simba, amepata dili la kwenda kukipiga
nchini Thailand.
Mghana huyo, hivi karibuni alitua kufanya majaribio Simba lakini alishindwa
kufuzu wakati mazoezi ya timu hiyo yakiwa yanasimamiwa na Mserbia, Goran
Kopunovic.
Geirson alifanya majaribio hayo kwa muda wa wiki moja kwenye
Uwanja wa Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam lakini akapigwa chini.
Meneja wa mchezaji huyo, Gibby
Kalule, alisema mshambuliaji huyo ametimkia Thailand Ijumaa iliyopita akitokea
Nairobi, Kenya alipokwenda kuchukua viza.
Gibby alisema, amekwenda nchini humo kwa ajili ya majaribio baada ya
kupata ofa kwenye klabu moja ambayo ni mapema kuitaja kwa hivi sasa.
“Ametokea Nairobi, Kenya alipokwenda kuchukua viza ya kuelekea
huko, upo uwezekano mkubwa wa kufuzu majaribio hayo,” alisema Gibby.







0 COMMENTS:
Post a Comment