June 25, 2015


Kiungo wa Simba, Jonas Mkude anaondoka leo kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio.


Mkude anakwenda kufanya majaribio katika klabu ya Bidvets ya Afrika Kusini.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema uongozi umempa ruksa na tayari umezungumza na uongozi wa benchi la ufundi la Taifa Stars.

“Tumemoa ruhusa Mkude aende kwenye majaribio, kwa kuwa amechaguliwa timu ya taifa, nao tumewasiliana nao.

“Kocha Mkwasa ni kati ya watu ambao wangependa maendeleo ya wachezaji kwenda nje, hii pia itaisaidia Taifa Stars. Hivyo hawezi kuwa na tatizo,” alisema.


Majaribio yanaweza kuwa ya wiki moja hadi zaidi kulingana na mahitaji ya timu hiyo inayomilikiwa na moja ya vyuo vikuu vikongwe barani Afrika cha Wits cha jijini Johannesburg.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic