Kama ulidhani Mwadui
Football club wanafanya utani, basi ujue unajidanganya maana sasa wamemsajili
straika tegemeo wa Mbeya City, Paul Nonga.
Nonga amemsajili Nonga
ambaye aliwahi kuichezea ikiwa daraja la tatu klabla ya kuondoka na kujiunga na
JKT Oljoro ya Arusha.
Nonga amejiunga leo na
Mwadui FC ingawa haijaelezwa mkataba huo utakuwa ni wa muda gani kama ni mwaka
mmoja au miwili.
Saa chache zilizopita,
Mwadui FC inayofundishwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ imemsajili beki wa Mbeya
City, Anthony Matogolo.
Benchi la ufundi la
matajiri hao wa Mwadui kutoka mkoani Shinyanga linaonyesha limepania
kujiimarisha mara tu baada ya kupanda Ligi Kuu Bara.
Mwadui FC ni kati ya
timu zilizokuwa katika daraja hilo katika miaka ya 1980. Sasa imerudi tena na
inaonekana imepania kuleta ushindani hasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment