Pamoja na kikosi cha Ruvu Shooting kushuka
daraja, uongozi wa Maafande hao umefunguka kuwa haupo tayari kumpeleka beki
wake, George Michael ‘Beki Katili’ katika timu yoyote hata kama ya jeshi kwa
sababu bado wana mkataba naye.
Awali iliripotiwa kuwa JKT Ruvu ilipeleka
maombi kwa ajili ya kumuomba beki huyo kuongeza nguvu kwenye kikosi chao msimu
ujao.
Ofisa habari wa timu hiyo, Masau Bwire
alifunguka kuwa beki huyo watashuka naye na hakuna timu ambayo inaruhusiwa
kumchukua.
Bwire alisema kuwa katika kikosi chao
kilichoshuka ni wachezaji sita tu ambao siyo waajiriwa wa jeshi ndiyo wapo huru
baada ya mikataba yao kumalizika.
“Beki George Michael hatuna mpango wa kumtoa
kwenda kwenye kikosi chochote ni mchezaji wetu halali na ana mkataba.
Haijalishi kuwa ni timu ya aina gani huyu tutakuwa naye daraja la kwanza msimu
ujao.
“Wachezaji ambao wapo huru mpaka sasa
kwenye kikosi chetu wapo kama Juma Nade, Stephano Mwasyika, Juma Kijiko, Jerome
Lambele na Salvatory Ntebe licha ya uongozi kutosema lolote kama wataendelea
nao au la, kwa hiyo kama timu inahitaji ifanye mazungumzo na hao,” alisema
Masau.
0 COMMENTS:
Post a Comment