Mshambuliaji nyota wa TP Mazembe, Mtanzania, Mbwana
Samatta amesema atarejea na kucheza nchini baada ya miaka 20 ijayo.
Samatta amesema angependelea kuendelea mbele zaidi
kisoka katika nchi nyingine za Afrika au Ulaya, halafu kama ni nyumbani
Tanzania, atarejea baada ya miaka 20.
“Baada ya miaka 20, nitarudi na kucheza hata kama ni
bure. Wakati huo nitakuwa nimemaliza mambo yangu.
“Kuna ofa kutoka katika timu mbalimbali za Ulaya na
Afrika, lakini bado sijajua itakuwaje,” alisema Samatta.
Mtanzania huyo ndiye tegemeo la Tanzania katika kikosi
cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Pia ndiye tegemeo katika kikosi cha wababe hao wa DR
Congo, TP Mazembe kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupachika mabao.
0 COMMENTS:
Post a Comment