Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) sasa limeamua kuliingilia sakata la
Simba na kiungo wake mshambuliaji, Ramadhani Sinagano.
Singano maarufu kama Messi analalamika kwamba mkataba wake na Simba ni
wa miaka miwili na umemalizika msimu uliopita, yaani 2014-15.
Lakini Simba imekuwa ikisisitiza kwamba ina mkataba wa miaka mitatu na
kiungo huyo na utafikia tamati msimu wa 2015-16.
Sakata hilo tayari limezua gumzo kubwa karibu kila sehemu ambayo michezo
ya Tanzania inasikika na hasa soka.
Lakini TFF imesema imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa
kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano wa klabu ya Simba.
“TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba
wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 9 mwezi huu kwa mazungumzo ili
kufikia mwafake,” alisema Msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto.
“Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake.
Ila katika kipindi
hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na
kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya
katika familia ya mpira wa miguu Tanzania.”
Issue hii ya Singano kuna mtu ataumbuka tu let's wait
ReplyDelete