June 26, 2015

HII NI ABAJALO YA SINZA, DAR ES SALAAM, SI ILE YA TABORA.
Abajalo FC ya Tabora, Alliance FC (Mwanza), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Madini SC (Arusha), na Sabasaba United FC (Morogoro) ndizo timu zilizopanda kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016.


Timu hizo zimepanda daraja baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyomalizika hivi karibuni kwenye vituo vya Lindi, Manyara na Rukwa na kushirikisha jumla ya timu 27.

SDL inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi manne inatarajia kuanza kutimua vumbi Oktoba 17 mwaka huu. Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, na timu itakayoongoza kundi ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2016/2017.

Kundi A lina timu za Abajalo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam), Milambo FC (Tabora), Mvuvumwa FC (Kigoma), Singida United (Singida) na Transit Camp (Dar es Salaam) wakati Kundi B ni AFC (Arusha), Alliance FC (Mwanza), Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma FC (Mara), Madini SC 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic