Wakali wa Golden State Warriors, wamefuta ndoto za mchezaji nyota wa
kikapu LeBron James kwa kubeba ubingwa wa NBA.
Warriors wameifunga Cleveland Cavaliers kwa pointi 105-97 katika mechi yake ya mwisho ya faiinali na
kubeba ubingwa.
Wakati Warriors wakichukua ubingwa huo kwa mara ya kwanza baada ya miaka
40, LeBron ameupoteza kwa mara ya nne akiingia fainali bila kuuchukua.
Ushindi wa Warriors unaifanya iibuke na ushindi wa 4-2 katika mechi sita
za fainali uliozikutanisha timu hizo. Cleveland Cavaliers walitaka kushinda
mchezo wa jana ili kufanya matokeo yawe 3-3 na klusababishwa kuongezwa kwa
mchezo mwingine wa fainali, lakini ikashindikana.
Stephen Curry wa Warriors ndiye ameibuka na tuzo ya mchezaji bora wa NBA
wa michezo yote ya fainali pamoja na Andre Iguodala.
Pamoja na kuukosa ubingwa huo, LeBron ameonyesha ni mmoja wa wachezaji
bora kabisa wa mchezo huo baada ya kuitoa Cleveland Cavaliers ikionekana timu
isiyo na makali hadi kucheza fainali. Katika mechi hiyo ya mwisho alifunga
pointi 32.












0 COMMENTS:
Post a Comment