Baada ya APR kufanikiwa kutinga robo fainali ya
Kombe la Kagame, kocha msaidizi wa timu hiyo, Mashami Vincent, ameibuka na
kusema hatua waliyofikia imethibitisha kwamba hawamtegemei aliyekuwa kiungo
wao, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’.
Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, kulikuwa na
hofu kuwa kutokuwepo kwa Migi aliyejiunga na Azam FC, kungeweza kuidhoofisha
APR katika Kombe la Kagame.
APR ilijitahidi kuomba kumtumia Migi katika
michuano hiyo lakini mambo yalishindikana na sasa anaichezea Azam.
Timu hiyo ya Rwanda imetinga robo fainali baada
ya kushinda mechi tatu mfululizo katika Kundi B na kujikusanyia pointi tisa
ikifuatiwa na A Ahly Shandy yenye pointi nne.
Vincent alisema: “Siku zote APR ni timu imara
licha ya kuwa tulipigwa vijembe vingi baada ya Migi kutimkia Azam, walisema tusingeweza
kufika popote kwenye michuano hii.”
“Siyo Migi tu, kuna wachezaji waliondoka na
tukawa imara, kumbuka kuhusu Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na hata marehemu
Patrick Mafisango.”
Wanga, Kavumbagu hawana uhakika ‘first eleven’
Azam
0 COMMENTS:
Post a Comment