MUKUNZI |
Yanga imesema inapambana kuhakikisha inamsajili
kiungo mkabaji wa APR, Yannick Mukunzi ili kujiimarisha katika michuano ya
kimataifa msimu ujao.
Mukunzi anayevaa jezi namba sita, anafanya vizuri
kwenye kikosi cha cha APR inayomilikiwa na Jeshi la Rwanda ambapo sasa viongozi
wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha inamsajili kiungo huyo.
Mmoja wa mabosi wa Yanga anayeshughulikia
usajili, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, Mukunzi anaweza kusajiliwa ili
kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite kutokana na gharama za kuwa naye kuwa kubwa.
“Tunataka kumsajili Mukunzi ili atusaidie
katikati kwani tumeona kuna tatizo katika kiungo mkabaji na hata Twite
anatumika ndivyo sivyo.
“Hata gharama za kuwa na Twite ni kubwa mno
kwani kila mwaka tunapaswa kuilipa FC Lupopo dola 10,000 (Sh milioni 20) kama
mkataba unavyosema, kwa hiyo kama tukifanikiwa kumsajili Mukuzi atachukua
nafasi ya Twite ikishindikana basi,” alisema bosi huyo.
Hata hivyo awali kumekuwa na taarifa kwamba, Yanga
inasaka beki kutoka katika Kombe la Kagame ili aongeze nguvu katika michuano ya
kimataifa.
Ukiacha Cannavaro na Yondani, mabeki wengine wa
kati wa Yanga ni Pato Ngonyani, Rajab Zahir anayetarajiwa kutolewa kwa mkopo na
kiraka Mbuyu Twite.
Wakati huohuo, straika wa Kpah Sherman
anatarajiwa kuondoka kesho Jumapili kwenda Afrika Kusini kufanya vipimo katika
Klabu ya Mpumalanga Black Aces ili aweze kujiunga nayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment