Mashabiki kibao wamejitokeza kwenye mazoezi ya
Simba yanayofanyika kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa na kusifia kiwango
kinachoonyeshwa mazoezini hapo.
Simba ipo visiwani hapa ikijiandaa na Ligi Kuu
Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 12, mwaka huu.
Kocha wa Simba, Dylan Kerr, akiwapa mazoezi
makali wachezaji wake kama kupiga mashuti makali langoni huku akiwasisitiza
kucheza kwa kupasiana.
Mashabiki ambao walijitokeza walikuwa wakipiga
makofi mara kwa mara kuonyesha kuwa wanamkubali Kerr, raia wa Uingereza, ambaye
amejiunga na Simba hivi karibuni.
Hata hivyo, mashabiki waliapa kuwa watakapocheza
mechi za kirafiki na timu za visiwani hapa, basi hawataishangilia Simba bali
watazipa sapoti timu za Zanzibar.
0 COMMENTS:
Post a Comment