July 25, 2015

Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche ameondoka na mpira baada ya kupiga bao tatu maarufu kama hat trick wakati Azam DC ilipoitwanga Adama City ya Ethiopia kwa mabao 5-0.
Katika mechi hiyo ya michuano ya Kombe la Kagame, tayari Azam FC ilishatinga robo fainali lakini ikaonyesha soka la kuvutia na kuwazidi kabisa Wahabeshi hao.
Azam FC ingeweza kupata mabao zaidi lakini mara kadhaa, Ame Ali na Kipre walipoteza nafasi kadhaa za kufunga.

Mabao mengine ya Azam FC iliyomaliza kundi C yalifungwa na Aggrey Morris na kiungo kinda Mudathir Yahya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic