Na Saleh Ally
MARAIS wa Afrika
ni kati ya wanaolipwa zaidi ikiwezekana hata kuliko wale wa Ulaya. Lakini
imekuwa ikielezwa kwamba wana posho zao za pembeni zinazowafanya wapate fedha zaidi.
Yote yanawezekana
na mfano mzuri ni ule wa Rais Teodoro Nguema wa Equatorial Guinea aitwaye
Obiang’ Mangue aliyetumia hadi dola milioni 315 kwa manunuzi ya samani na vitu
vingine vya kifahari kuanzia mwaka 2004 na 2011.
Mangue ni waziri,
kwa mwaka mshahara wake ni dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni 210). Hivyo
mshahara unaweza usiwe kitu kwa marais wa Afrika.
Lakini kama
utazungumzia kila kitu kiende kwa utaratibu, halafu kama kweli wanaotaka urais
inakuwa ni kwa ajili ya kufuata maslahi, basi ingekuwa ni bora wote wakacheza
mpira na kutafuta mafanikio ya kukipiga Ulaya ambako wangelipwa zaidi.
Wanasoka wa
Afrika wanaocheza barani Ulaya wanaonekana kulipwa fedha nyingi kuliko marais
wa nchi zao.
Pamoja na kuwa
nchi yake ni ndogo, lakini Rais wa Cameroon, Paul Biya, ndiye anaongoza kwa
kulipwa zaidi kuliko marais wengine wote wa Afrika kwa kuwa kwa mwaka anachukua
dola 630,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.3).
Hiyo inashangaza
kwa kuwa Biya anamshinda Jacob Zuma wa Afrika Kusini kwa mshahara licha ya kwamba
nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika inaizidi Cameroon mara 10 kiuchumi.
Kwa yeye Biya
anachukua mshahara mara 229 dhidi ya wananchi wa kawaida, hasa waajiriwa wa
serikalini. Huku Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf akiwa anachukua mara
113 zaidi ya wananchi wa kawaida.
Usishangae, Rais
wa Somalia, Sheikh Hassan Mohamoud anayechukua dola 120,000 kwa mwaka pia ni
kati ya marais wanaolipwa vizuri.
Kwa mujibu wa
Daily Mail na Dail Nation, inaonyesha Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
anachukua dola 192,000 (Sh milioni 405) kwa mwaka na kumfanya ashike nafasi ya
nne kwa marais wanaolipwa vizuri Afrika.
Kikwete
anafuatiwa na Obiang’ Mangue wa Guinea ya Ikweta halafu Uhuru Kenyatta wa Kenya
anayechukua 132,000 na marais hawa wawili wa Afrika Mashariki ndiyo pekee walio
katika 10 bora ya wanaolipwa vizuri zaidi.
Kinachovutia
zaidi ni kwamba ni hivi, pamoja na ukubwa wa marais hao, lakini wachezaji
wanaokipiga Ulaya katika Ligi Kuu za England, Italia, Hispania na Ujerumani,
wanalipwa vizuri zaidi ya wakubwa hao wa nchi.
Mfano Rais wa
Ivory Coast, Allasane Ouattara anachukua mshahara wa dola 100,000 kwa mwaka, fedha
ambazo Yaya Toure wa Manchester City anazipata kwa wiki tena mara tatu yake na
ushee kwa kuwa analipwa pauni 240,0000 kwa wiki ambayo ni zaidi ya Sh milioni
789.
Kwa mwaka Toure anaingiza pauni milioni 13,
fedha ambazo ni zaidi ya mara 24 anazolipwa rais wake ambaye ndiye kiongozi
wake wa nchi.
Kama utazungumzia
kwa kiongozi wetu wa nchi, Toure anachukua zaidi ya mara 18 ya fedha anazolipwa
kwa mwaka.
Hii inaonyesha
kiasi gani mchezo wa soka ambao hauhitaji mtu kupata elimu ya chuo kikuu, unaweza
kukuletea mafanikio makubwa.
Kipaji ndiyo,
lakini juhudi kuu pamoja na nia ya kutimiza kitu kikubwa ndiyo sehemu ya
mafanikio makubwa.
Mshambuliaji wa
TP Mazembe, Mbwana Samatta, analipwa dola 120,000 kwa mwaka kupitia mshahara
wake wa mwezi. Utaona tofauti ya Samatta na Rais Kikwete ni dola 72,000. Fedha
ambazo baada ya muda mchache ujao kama Samatta atapata nafasi ya kucheza Ulaya,
basi atazipata na zaidi.
Mifano hiyo ya
wanachoingiza marais wa Afrika na wachezaji wanaocheza Ulaya kwa wao kuonekana
wana fedha nyingi zaidi inaweza kuwa changamoto kubwa kwa viongozi wa Tanzania
na Afrika kwa ujumla.
RAIS ZUMA |
Wanapaswa kujua
michezo na hasa soka, inalipa na inasaidia kupatikana kwa ajira ya uhakika.
Kwani hata kama wachezaji hawatalipwa kama akina Yaya, Didier Drogba na Samuel
Eto’o lakini wana nafasi ya kupata ajira kubwa kuliko mawaziri au mabosi wa
makampuni makubwa ya serikali, pia yale ya binafsi.
Tanzania ihame
kutoka kuufanya mchezo wa soka kama sehemu ya kujiburudisha au watu wengine
kupata nafasi ya kuwatania wengine baada ya kufunga, badala yake uwe kwenye
programu za nchi kuuendeleza na kuufanya uisaidie nchi kuwasaidia vijana
wajiajiri kwa kuwa si kila mmoja atasoma na kupata digrii.
MSHAHARA WA
WIKI MWAKA
1 Yaya Toure (Man City) £240,000 £13.5m
2 Asamoah Gyan (Al-Ain) £120,00 £7.5m
3 Emmanuel Adebayor (Spurs) £101,000 £5.4m
4 Samuel Etó’o (Everton) £80,000 £4.2m
5 Didier Drogba (Chelsea) £75,000 £3.8m
6 Mikel John Obi (Chelsea) £75,000 £3.8m
7 Michael Essien (AC Milan) £60,000 £2.9m
8 Christopher Samba (Dynamo) £60,000 £2.9m
9 Kolo Toure (Liverpool) £60,000 £2.9m
10 Seydou Keita (AS Roma) £55,000 £2.9m
MISHAHARA YA MARAISI MWAKA
1. Paul Biya (Cameroon) $ 630,000
2. King Mohammed (Morocco) $ 480,000
3. Jacob Zuma (Afrika Kusini) $ 272,000
4. Jakaya Kikwete $192,000
5. Abdelaziz Bouteflika (Algeria) $168,000
6. Obiang’ Mangue (E. Guinea) $150,000
7. Uhuru Kenya (Kenya) $132,000
8. Ikililou Dhoinine (Comoro) $115,000
9. Denis Sassou Nguesso (Congo) $110,000
10. Hage Geingob (Namibia) $110,000
11. Roberto Mugabe (Zimbabwe)
$108,000
12. Ameena Gurib (Mauritius) $104,000
13. Allasane Ouattara (Ivory Coast)
$100,000
14. llen Johnson Sirleaf (Liberia)
$90,000
15. Paul Kagame (Rwanda) $85,000
0 COMMENTS:
Post a Comment