Winga wa
Manchester United, Angel di Maria anajiandaa kuondoka England na kwenda
kuishi Uafaransa ambako atafanya kazi na PSG.
Kocha Louis van
Gaal tayari amewaambia wachezaji kwamba Di maria anaondoka.
Raia huyo wa
Argentina ameonekana kutokuwa na furaha na maisha ya Manchester United. Sasa milango
iko wazi kwake kuondoka.
Taarifa zinasema
mabingwa hao wa Ufaransa yaani Paris Saint-Germain wako tayari kumnasa kwa
kitita cha pauni milioni 46.5.
United
inaonekana kutomfurahia kwani itamuacha atue PSG kwa hasara, maana ilimsajili
kwa pauni milioni 59.7 kutoka Real Madrid na ameitumikia kwa msimu mmoja tu!
0 COMMENTS:
Post a Comment