Kocha wa Yanga,
Hans van der Pluijm amesisitiza kwamba leo wanataka ushindi hata kama wamevuka
na kuingoa robo fainali.
Yanga inashuka
dimbani leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwavaa Al Khartoum ya
Sudan katika mechi ya kukamilisha ratiba ya makundi hatua ya Kagame lakini
tayari imefuzu robo fainali baada ya ushindi wa mechi mbili na kupoteza moja.
“Ushindi una
mambo mawili makubwa, kwanza tunataka kupata pointi tisa na kujiinua kimorali
kwamba tuna kikosi kinachoweza kupambana.
“Pili tunataka
kupata pointi tisa ikiwezekana kukwekea nafasi za juu yaani moja au mbili
katika kundi,” alisema Mholanzi huyo.
“Kweli
tumevuka, lakini kuruhusu kufungwa kwa mara ya pili katika mechi nne, litakuwa
ni tatizo.
“Tuko katika
kipindi cha kutengeneza timu na tunahitaji kurudisha imani kwa mashabiki na
kuinua morali yetu,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment