Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premieum Lager imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The Cranes)
katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017 nchini Rwanda
uliofanyika uwanja wa Nakivubo.
Stars
ambayo leo imeonekana kabadilika katika mchezo wa leo, ilicheza soka la kuvutia
tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaduwaza wenyeji Uganda.
Mpaka
dakika 45 za mchezo za kipindi cha kwanza zinamalizika, Uganda 0 - 0 Tanzania.
Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi mfululizo kupitia kwa
washambuliaji wake John bocco na Rashid Mandawa.
Dakika
ya 58, John Bocco aliipatia Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju wa penayi
kufuatia mlinzi wa Uganda Bakaki Shafik kuunawa mpira wa ndani ya eneo la
hatari.
Mara
baada ya bao hilo Uganda walifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Stars na
kufanikiwa kupata bao la kusawzisha dakika ya 82, kupitia kwa mchezaji Kizito
Hezron.
Mpaka
dakika 90 za mchezo zinamalizika Uganda 1 - 1 Tanzania. Kwa matokeo hayo Uganda
wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 - 1 na sasa watakutana na
Sudan.
Mara
baada ya mchezo huo kochaa mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema
anashukuru vijana wake wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo ulikua mzuri timu
ilitengeneza nafasi chache na kuweza kutumia nafasi moja iliyopatikana.
Mkwasa
amewaomba watanzania kuendelea kuwapa sapoti, wamekaa na timu kwa muda mfupi wa
wiki moja tu lakini katika mchezo wa leo mabadiliko yameonekana, hivyo wanahitaji
muda kidogo kuweza kukaa na vijana kwa muda mrefu ili kujenga timu bora.
Stars
inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la
ndege la Rwanda Air.
Taifa
Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub, Kelvin
Yondani, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo,/Said Ndemla John Bocco,
Rashid Mandawa/Salum Telela, Saimon Msuva/Ramadhan Singano.
The
Cranes: James Alitho, Muzamiru Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan Waswa, Denis Oola,
Faruk Miya, John Shemazi/Robert Sentongo, Bakaki Shafik, Tekkwo Derick/Kizito
Hezron/Kalanda Frank.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 COMMENTS:
Post a Comment