Mwenyekiti wa Kimondo, Erick Ambakise ameibuka na kusema TFF iwe makini katika suala la Geofrey Mwashiuya.
Ambakise ameonyesha mkataba wa miaka mitatu waliosaini na Mwashiuya na kuonya kuwa TFF inapaswa kuwa makini na kulimaliza suala hilo kabla ya kumuidhinisha aichezee Yanga.
"Mkataba wetu wa miaka mitatu na Mwashiuya tumeuweka hadharani, hivyo wawe makini sana na waungalie mkataba huo," alisema.
Yanga na Kimondo zimeingia katika mgogoro mkubwa huku Kimondo ikitaka malipo kwa kuwa ina mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19.
Lakini Yanga imekuwa ikisisitiza kwamba Mwashiuya, hana mkataba na Kimondo na inapaswa kuachwa iendelee na mambo yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment