Beki wa zamani wa Simba, Donald Musoti, amesema ili Yanga ifanye vizuri katika mchezo wake wa Kombe la Kagame wiki ijayo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, ni lazima iwachunge zaidi Meed Kagere na Michael Lunga.
Kauli hiyo ya Musoti imekuja saa chache baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kusema halina taarifa juu ya Gor Mahia kutishia kujiondoa katika Kombe la Kagame linaloandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
Yanga imepangwa Kundi A sambamba na Gor Mahia, KMKM na Telecom na itacheza mechi yake ya kwanza Julai 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya timu hiyo ya Kenya.
Akizungumza kutoka Nairobi Musoti alisema: “Iwapo Yanga inataka kuibuka na ushindi katika mchezo huo, lazima ihakikishe inawazuia Kagere na Lunga na kutopata mpira kwenye eneo la hatari.
“Kama Yanga wakizubaa na kuendelea kucheza kama nilivyowaacha, basi wataumia kwa hawa wachezaji wawili, hivyo inabidi wafanye mazoezi ya kuwazuia na wasiwaache hovyo siku ya mechi.”
Alisema kwa sasa washambuliaji Kagere na Lunga ndiyo wachezaji muhimu na hatari katika kikosi cha Gor Mahia.
0 COMMENTS:
Post a Comment