Kiungo
mshambuliaji anayefanya mazoezi na Azam FC, Ryan Burge, raia wa Uingereza,
ataikosa michuano ya Kombe la Kagame ambayo inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi
kutokana na kanuni za michuano hiyo kumbana.
Burge
ambaye alitua nchini hivi karibuni na kuanza mazoezi chini ya Kocha Stewart
Hall ambaye ni Mwingereza mwenzake, atakosa michuano hiyo kwa kuwa hajasajiliwa
na kanuni za michuano hiyo inayosimamiwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika
Mashariki na Kati (Cecafa), zinasema kuwa wanaoruhusiwa kushiriki ni wale
waliosajiliwa na klabu husika.
Ofisa
Habari wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga, ameliambia gazeti hili kuwa, mchezaji
huyo alikuwa kwenye mipango ya kocha wao lakini ndiyo hivyo atakosa michuano
hiyo kwa kuwa hawana jinsi.
“Tutawakosa
baadhi ya nyota wetu akiwemo Burge licha ya kuwa yupo katika mipango ya kocha,
bado hajasaini mkataba,” alisema Maganga.
Aidha, Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Baraka Kizuguto, naye alisisitiza juu ya kanuni hiyo kwa kusema:
“Wachezaji ambao wapo kwenye majaribio ya timu shiriki hawataruhusiwa kucheza
Kombe la Kagame. Wanaoruhusiwa ni wale wenye mikataba rasmi.”







0 COMMENTS:
Post a Comment