Simba ipo
kambini Lushoto, Tanga kujiandaa na msimu wa 2015/2016, kuna mengi yanaendelea
kambini huko lakini kuhusu Kocha wa Simba, Dylan Kerr ni habari nyingine, sikia
hii mpya aliyoitoa.
Licha ya
kuwa kocha huyo ni mgeni nchini Tanzania, lakini ameonyesha kuwa ni mwepesi wa
kuijua mitaa pindi anapotembelea au kukaa hata kama ni kwa muda mfupi, hiyo ni
baada ya kumzidi mwenyeji wake katika kuzijua njia za Tanga.
Kerr
ambaye pia amekuwa mstari wa mbele kuwaongoza wenzake wanapokuwa matembezini
kama vile ni mwenyeji wa Tanga, mapema wiki hii alimzidi ujanja msaidizi wake,
Selemani Matola wakati walipokuwa wakibishana juu ya njia ya kupita.
Ilikuwa
hivi, Kerr na Matola walitembelea Gereza la Lushoto, walipokuwa wakirejea
kambini kwao umbali wa kama kilometa nne kutoka gereza lilipo, walianza
kubishana walipofika katikati ya safari juu ya njia ipi wapite ili wafike
kambini kwao.
Baada ya
kuvutana kwa muda, wakaona isiwe tabu, wakaamua kuwauliza wenyeji wao juu ya
njia sahihi ni ipi kuelekea kambini kwao, Kerr akaibuka mshindi kwa kuwa njia
waliyoelekezwa ni ile ambayo yeye ndiye alikuwa akitaka wapite.
Matola
akawa mpole na safari ikaendelea kama kawaida huku wazawa hao wakibaki na
maswali mengi jinsi Mzungu huyo alivyoweza kukariri njia kwa muda mfupi huku
wengine wakijiuliza: “Au ameshawahi kufika Tanga?”








0 COMMENTS:
Post a Comment