Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amepata nafasi ya
kuiona Yanga ikicheza kwa mara ya kwanza katika mashindano.
Kerr raia wa Uingereza alikuwa uwanjani wakati Yanga
ikipambana na Gor Mahia ya Kenya na kupoteza kwa mabao 2-1.
Kerr amesema, Yanga ni timu nzuri lakini si tishio
kama alivyokuwa akisikia.
“Ni timu nzuri na inaweza kutoa ushindani, lakini si
kama vile nilivyoambiwa,” alisema.
“Kwa kuwa nimeiona, nitaendelea kuangalia zaidi
wanavyocheza. Pia ningependa kuiona Azam FC katika mechi zake maana ndiyo
wapinzani wenyewe,.”
Kerr ameishaanza kuinoa Simba na ilikuwa kambini
wilayani Lushoto kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam.
Chini yake, Simba bado haijaanza kucheza mechi za
kirafiki kujiweka vizuri.







0 COMMENTS:
Post a Comment