Wakati
Chelsea ikiwa nchini Canada kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, Kocha wake,
Jose Mourinho, amesema wala haoni shida namna timu nyingine zinavyokimbizana
kwenye usajili.
Mourinho
amesema Chelsea haiwezi kufanya usajili kwa kuangalia nani amefanya kitu gani.
“Kweli
wenzetu wanatumia fedha nyingi katika usajili, lakini hiyo ni mipango yao na
yetu ndiyo hii tunayofanya.
“Tunajua
tunafanya nini, tunajua tunataka nini hivyo hatuna sababu ya kufuata mkumbo,”
alisema.
Chelsea
ndiyo mabingwa watetezi wa England na msimu huu ni kati ya timu zilizosajili
wachezaji wachache zaidi huku Mourinho akisisitiza kutaka kubaki na kikosi cha
msimu uliopita kwa zaidi ya asilimia 90.











0 COMMENTS:
Post a Comment