Kocha wa zamani wa
Simba, Talib Hilal ametua nchini na kufanya ziara fupi kwenye ofisi za gazeti
la Michezo la Championi.
Hilal ambaye sasa
ni kocha wa timu ya taifa ya ufukweni ya Oman alitembelea Championi na
kuzungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa gazeti hilo namba moja la michezo
nchini.
Talib alijibu
maswali kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo na ushauri.
Kocha huyo
aliyewahi kuipa Simba ubingwa wa Tanzania Bara, aliongozana na straika hatari
wa zamani wa Simba, Bitha John Musiba ambaye pia alipata nafasi ya kutoa
mafunzo kwa waandishi na wahariri wa Championi.
BHITA JOHN (KUSHOTO) AKIFAFANUA JAMBO KWA WAHARIRI WA CHAMPIONI. KATIKATI NI SALEH ALLY NA KULIA NI TALIB HILAL. |
Hivi karibu, Talib
alikuwa nchini Ureno akiingoza Oman kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la
soka la ufukweni.
Kabla ya hapo,
kocha huyo mwenye asili ya Tanzania alikuwa ameipa Oman ubingwa wa Asia wa soka
la ufukweni na kuwapiga vikumbo vigogo Japan na Iran.
0 COMMENTS:
Post a Comment