Kocha
Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kesho watapambana vilivyo
kuhakikisha wanaitwanga Al Kharthoum.
“Kama
tutafikisha pointi tisa, basi tuna nafasi ya kuongoza kundi. Tutafanya hivyo
bila ya kujali nani atafanya nini katika mechi nyingine,” alisema.
“Kwa kweli
tumejiandaa vizuri sana, wachezaji wanajua tunachotaka kufanya kesho na wao
wako tayari,” aliongeza Mkwasa.
Yanga
imepoteza mechi moja na kushinda mbili, hivyo tayari imefuzu robo fainali
lakini inataka kujiweka vizuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment