Kikois cha Neckarsulmer kinachoshiriki Ligi Daraja la
Tano nchini Ujerumani kimeanza kwa kasi michuano ya Kombe la Ujerumani baada ya
kushinda kwa mabao 5-0 dhidi ya Gröningen-Satteldorf 1946.
Mtanzania Emily Mgeta ambaye ni beki wa kushoto amefanikiwa kufunga bao
moja na kutoa pasi mbili za mabao.
Mgeta aliyewahi kuichezea Simba amezungumza na SALEHJEMBE na kusema
mechi ilikuwa ngumu, ila ana furaha.
“Nina furaha sana kwa kuwa nimecheza vizuri, nimetoa pasi mbili na
kufunga bao moja.
“Lakini kizuri zaidi safu ya ulinzi, mimi nikiwa mmoja wao,
hatujafungwa,” alisema Mgeta.
0 COMMENTS:
Post a Comment