July 27, 2015


Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limeiandika barua ya onyo klabu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya kufuatia kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu katika michezo yake miwili ya kwanza.


Katika barua hiyo ya Cecafa kwenda kwa Gor Mahia, imeutaka uongozi huo kuhakikisha kocha wake Frank Nutal na kikosi kizima kinafuata taratibu za mashindano na kanunu zilizopo zinazoongoza michuano hiyo.

Kamati ya uendeshaji wa michuano hiyo (LOC) iliwasilisha malaliko kwa uongozi wa Cecafa juu ya tabia ya utovu wa nidhamu iliyoonyeshwa na kocha mkuu wa Gor Mahia, na kitendo cha kuvunja kitasa cha mlango ili kuingia uwanjani.

1 COMMENTS:

  1. Kwanini musonye abadharau mpira wa tanzania namna hiyo!! Zingekuwa timu za Tz hapo ingekuwa fine na kufungiwa juu lakini kwa sbb ni timu zao zinapewa onyo tu kwa matendo ya kihuni na uharibu wa uwanja!! It is time watanzania tuamke tuwakatae akina Musonye ambao kazi yao ni kuvuruga soka la bongo!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic