July 25, 2015


MWADUI FC.
Mwadui FC imesema inajitahidi sana kuomba mechi za kirafiki na klabu za Ligi Kuu Bara, lakini haizipati kwani kila timu inawagomea kujipima nayo.
Katibu Mkuu wa Mwadui, Ramadhan Kilao kila timu wanayoiomba mechi huwajibu kuwa bado wanaimarisha vikosi vyao na hawako vizuri kupambana kwa sasa.
Kilao amesema kuwa; “Tunahitaji michezo mingi ya kirafiki lakini kila tukiomba mechi kwa timu za ligi kuu tunakosa. Tumejaribu Toto African na Stand United kote imeshindikana, hivyo tunacheza na timu yoyote ili kujipima tu.”

Mwadui inayofundishwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ imesajili nyota kibao waliowahi kucheza Simba na Yanga akiwemo Athuman Idd ‘Chuji’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic