July 25, 2015

OLUNGA (KULIA) AKISHANGILIA NA WENZAKE WA GOR MAHIA...
Simba inapambana muda wote kuhakikisha inamsajili straika Michael Olunga wa Gor Mahia, lakini nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ni kama anataka kutibua dili hilo aliposema; “Huyo Olunga hana lolote, isipokuwa ana bahati tu.”


Cannavaro alienda mbali kwa kusema, siku Yanga ilipocheza na Gor Mahia ni kweli Olunga aliwasumbua na kufanikiwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-1 walioupata, lakini hana uwezo wa kusumbua katika ligi.
CANNAVARO
Cannavaro amesema: “Ujue siku ile tulipocheza na Gor Mahia, Olunga alikuwa na bahati na kweli alitusumbua lakini sidhani kama ana uwezo mkubwa kiasi cha kututisha.”

“Kwa kweli alibahatisha tu, nasikia Simba wanataka kumsajili. Waache wamsajili halafu tukutane naye katika ligi (Ligi Kuu Bara) ndipo watakapoona kama wanamsajili mchezaji wa kawaida tu.”


Cannavaro alisema anatamani wakutane tena na Gor Mahia katika mechi zijazo za Kombe la Kagame ili kuthibitisha kauli yake na kuwahakikishia Simba kwamba wanataka kusajili mchezaji wa kawaida.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic