August 9, 2015

NGASSA KABLA YA MECHI AKIWA VYUMBANI ...
Licha ya kucheza ugenini mjini Bethlehem, Mpumalanga Black Aces anayochezea mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Kpah Sherman imeibuka na ushindi wa bao 1-0.

Aces wameibuka na ushindi wa bao hilo moja katika mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL) dhidi ya Free State Star anayochezea mshambuliaji mwingine wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa.
MPUMALANGA WAKISHANGILIA BAADA YA BAO LA JAYIYA...
Ngassa alishindwa kuisaidia Free State Star iliyokuwa nyumbani na kujikuta ikiruhusu bao pekee lililofungwa na Jayiya.

Hata hivyo, kipa wa Aces, Jackson Mabokgwane aliibuka nyota wa mchezo kutokana na kufanya kazi ya kuzuia michomo ya Ngassa na wenzake.

Kipa huyo, mara mbili aliokoa mashuti ya Ngassa aliyekuwa amewatoka mabeki na kubaki naye, lakini 'akafanya maajabu'.

Baadaye Free State walilazimika kucheza pungufu baada ya beki wake kulambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu katika dakika ya 84 ikiwa ni baada ya kumuangusha Mzambia, Collins Mbesuma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic