Yanga ipo kambini jijini Mbeya kwenye baridi
kali lakini kocha wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm anaamini hali hiyo ya hewa
itawaweka fiti wachezaji wake kuweza kufanya vizuri katika mechi zao zijazo
ikiwemo dhidi ya Azam FC.
Agosti 22, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, Yanga itacheza na Azam mechi ya Ngao ya Jamii ambayo
hukutanisha timu bingwa wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara na iliyoshika nafasi
ya pili.
Yanga ambayo ni bingwa mtetezi ipo kambini
Mbeya ambako kesho Jumapili itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mbeya City
kwenye Uwanja wa Sokoine ili kujipima nguvu.
Pluijm, amesema: “Licha ya kuwepo
baridi, naamini hiyo ni njia mojawapo ya kuwajenga wachezaji wangu huku
tukihakikisha tunapunguza makosa yanayojitokeza mara kwa mara kwenye kikosini
chetu.”
Tayari Yanga imecheza mechi mbili za kirafiki ikiwa Nyanda za Juu, Kusini na kushinda zote ikianza kwa kuitandika Kimondo kwa mabao 4-1 kabla ya kuituliza Prisons kwa mabao 2-0.
Imebakiza mechi moja dhidi ya Mbeya City ambayo ndiyo timu ngumu zaidi katika ukanda huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment