August 15, 2015


Siku chache baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa Super Cup, Barcelona wamekiona cha moto baada ya kukutana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Athletic Bilbao katika mechi ya kwanza.

Swali ni hivi, kweli Barcelona wataweza kurudisha mabao hayo manne na kushinda dhidi ya Bilbao katika mechi ya pili itakayoamua bingwa pale Camp Nou? 

Licha ya kuwemo kwa nyota Lionel Messi, Bilbao wametoa adhabu hiyo kwa Barcelona katika mechi ya Super Cup ya Hispania.

Hadi mapumziko, Bilbao walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mikel San Jose aliyefunga katika dakika ya 13.

Huku ikionekana Barcelona ingerejea na kujirekebisha katika kipindi cha pili kama ilivyofanya kwenye mechi ya Uefa Super Cup dhidi ya Sevilla baada ya kutangulia kufungwa na kusawazisha, haikuwa hivyo.

Kwani Bilbao ndiyo walizidi kupaa na kufunga mabao ya harakaharaka baada ya Artiz Aduriz kufanya mabao mawili ya fasta katika dakika ya 53 na baadaye 63.

Kitendo cha Bilbao kufikisha mabao matatu kilionekana kuwachanganya Barcelona, wakaendelea kushambulia mfululizo na kujisahau kufanya ulinzi mzuri.

Hali hiyo ilisababisha Bilbao kupata bao la nne kupitia Aduriz aliyekuwa anafunga lake la tatu au hat trick.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic