Kocha Louis van Gaal wa Manchester United
amekubali kuwa pamoja na kuanza ligi na
ushindi lakini hawako vizuri sana.
Van Gaal raia wa Uholanzi amesema Man United
inalazimika kujipanga zaidi ili kuboresha kiwango chake.
“Hakika tuna bahati, haikuwa lahisi. Tumeshinda
lakini lazima tujiimarishe zaidi katika sehemu mbalimbali.
“Hatukuwa katika kiwango kizuri tunachoweza
kusema tumeshinda na tuna kiwango bora,” alisema.
Man United imeanza Premier League kwa ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Tottenham ambao walijifunga.
0 COMMENTS:
Post a Comment