Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
linatarajia kumpeleka katika kamati ya maadili ya TFF Mwenyekiti wa kamati ya
uchaguzi ya DRFA, Rashid Saadallah siku ya Alhamisi tarehe 27/08/2015 saa
9:00 alasili kwa kosa la kudharahu na kupingana na maagizo ya mwenyekiti wa
kamati ya uchaguzi ya TFF.
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF alimwagiza
asimamishe uchaguzi wa chama cha mpira wa wilaya ya Temeke (TEFA), ili kuitisha
fomu zote za waomba uongozi pamoja na maamuzi ya kamati za TEFA na DRFA ili
kujiridhisha kama taratibu zilifuatwa katika mchakato huo kutokana na
malalamiko ya baadhi ya wagombea kwamba hawakutendewa haki.
Pamoja na kupata barua hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa
kamati ya uchaguzi ya TFF aliandika barua ya kukataa kutii maagizo hayo. TFF
imechukua hatua hiyo kulinda nidhamu kwa vyombo vilivyo chini ya TFF.








0 COMMENTS:
Post a Comment