September 29, 2015

Kipa nyota duniani, Gianluigi Buffon ameweka wazi mapenzi yake ya dhati kipa mwingine nyota, Iker Casillas.


Buffon amesema Casillas ni kipa bora kabisa kwa ngazi ya klabu na taifa, lakini anashangazwa na mambo yalivyobadilika kwake haraka na wengine kufikia kumvunjia heshima kwa kumzomea, jambo ambalo anaamini si sahihi hata kidogo.

"Navutiwa sana na Casillas, ameshinda kila kitu katika mpira. Anajua kila kitu katika mpira na amekuwa mtu bora na mpambanaji wa dhati.

“Anastahili heshima kubwa, kwangu hata kama angepiga mpira uingie langoni na kujifunza, bado hastahili kuzomewa, apigiwe makofi,” alisema Buffon.


Baada ya kuona mambo yake hayaendi vizuri na Real Madrid, Casillas aliamua kuondoka na kujiunga na FC Porto na leo atakuwa uwanjani timu yake ikicheza na Chelsea.

GAZETTA DE LA SPORT

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic